Update:

RAIA WA TUNISIA WASAINI HATI YA KUMPINGA RAIS

Chama cha al Mahabba nchini Tunisia kimeanza kukusanya saini za raia wa nchi hiyo katika mchakato wa kutaka Rais Mohamed Beji Caid Essebsi atimuliwe baada ya kutoa wito unaokiuka sheria za mirathi za Kiislamu.

Chama hicho kimetangaza kuwa, hadi sasa kimekusanya zaidi ya saini za watu laki moja na elfu ishirini kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa nchi hiyo.

Watu wanaosaini hati hiyo wametangaza upinzani wao dhidi ya matamshi yaliyotolewa na Rais Mohamed Beji Caid Essebsi kuhusu usawa wa mirathi baina ya mwanamke na mwanaume na wito wake wa kuruhusiwa ndoa baina ya wanawake wa Kiislamu na wasio Waislamu katika nchi ya Tunisa yenye idadi kubwa ya Waislamu.

Chama cha al Mahabba kimetangaza kuwa, kimeunda tume maalumu ya wanasheria ya kuchunguza njia za kumuondoa madarakani Rais Mohamed Beji Caid Essebsi wa Tunisia ikiwa ni pamoja na kuliwasilisha suala hilo bungeni kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.Mohamed Beji Caid Essebsi

Wito huo wa Rais wa Tunisa pia umepingwa vikali na wanazuoni na wasomi wa Kiislamu nchini humo. Mufti wa zamani wa Tunisia, Hamida Saiid amesema kuwa, suala la mgao wa mirathi katika Uislamu ni suala lililowekwa wazi katika Qur'ani tukufu na hadithi za Mtume (saw) na halihitaji tafsiri wala mabadiliko ya aina yoyote.

No comments