Update:

PSG yakubaliana na AS Monaco kumsajili kinda Kylian Mbappe

Timu ya Paris Saint-German (PSG) imefikia makubaliano na AS Monaco kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kinda Kylian Mbappe kwa mkopo wa mwaka mmoja ambapo hapo baadaye wanaweza wakamsajili moja kwa moja kwa ada ya pauni 166 milioni katika majira ya joto mwakani.

Baada ya kumsajili Neymar kwa ada ya usajili uliovunja rekodi ya dunia ya pauni 200 milioni kutoka Barcelona mwanzoni mwa mwezi huu, PSG itamsajili Mbappe kwa mkopo ili kuendana na sheria ya Financial Fair Play. Mbappe alizivutia klabu kubwa barani Ulaya kama Real Madrid, Barcelona, Manchester City, Liverpool pamoja na Arsenal lakini anaelekea kutua PSG.

No comments