Update:

Pazia la ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 lafunguliwa rasmi

Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 umeanza Jumamosi ambapo nyasi za viwanja kadhaa zilishuhudia mitanange ya mechi sita kwenye viwanja tofauti. Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Simba Sports Club imeibuka na ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Emmanuel Okwi mshambuliaji wa Simba alifungua pazia la Hat Trick ya kwanza. Matokeo mengine, Azam wameifunga Ndanda 1-0, Mbao FC imeshinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, Tanzania Prisons 2 -1 dhidi ya Njimbe Mji, huku Mwadui FC wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United, Mbeya City nao wamewafunga Majimaji 1-0, Mtibwa Sugar ikitoka sare na Stand United. Ligi hiyo imeendelea jana kwa mchezo mmoja kati ya Yanga na Lipuli, timu hizo zimetoka sare ya 1-1.