Update:

Neymar asema amezaliwa upya ndani ya PSGBaada ya kupata tuzo la mchezaji bora wa mechi kwa kutengeneza mabao mawili na kufunga moja dhidi ya Guingamp, Neymar ameanza kufurahia maisha ndani ya Paris Saint-Germain, akisema ameanza maisha Ufaransa huku kukiwa na shutuma kuhusu uamuzi wake wa kuondoka Barcelona.

Akiweka mbali kabisa na kusahau maisha Camp Nou, tayari Mbrazili huyo ameanza kujiona yuko nyumbani ndani ya Paris.

Neymar alidhibitisha kuwa amemetulia katika klabu yake mpya ya PSG. Alikiri kuwa ilikuwa vigumu kwake kuondoka Barcelona, lakini kwa sasa anasema amefurahi kuwa Ufaranza.

Alisema anafahamu kwamba wengi walifikiri kuondoka kwake Barcelona ndiyo mwisho wake, lakini mambo kulingana naye yamekuwa ni tofauti kwani katika PSG yeye anajiona kama mchezaji aliyezaliwa upya.

Mashambulizi huyo wa timu ya soka ya taifa ya Brazil anasisitiza kuwa anafurahi na kuendelea kucheza soka kwa kiwango kile kile, huku akibainisha kuwa kilichobadilika ni nchi, mji na timu tu.