Update:

Mwenyekiti wa kijiji cha Buchosa kata ya Nyehuge Boniphas Kadinda (Chadema) akamatwa
Jeshi la Polisi wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi katika Kijiji cha Mwabasabi Kata ya Nyehunge, lilipotaka kumkamata mwenyekiti wa kijiji hicho, Boniphas Kadinda (Chadema) akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali.

Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu, kijijini hapo baada ya polisi kufika katika mkutano huo na kudai ni batili kwasababu hauna kibali hivyo mwenyekiti huyo yupo chini ya ulinzi na kabla hawajamkamata wananchi waliokuwapo walizuia asikamatwe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema kukamatwa kwa mwenyekiti ni kwa mujibu wa sheria kwani amekuwa na tabia ya kuwakataa watendaji wa vijiji wanaokwenda kufanya kazi kijijini hapo akiwatuhumu kuwa walikotoka walikuwa wezi hivyo wasipokewe.

No comments