Update:

MTENDAJI WA KATA APIGA MARUFUKU KITENDO CHA WATOTO WADOGO KUTUMIKISHWA KIBIASHARAWito huo umetolewa na mtendaji wa kata ya levolosi jijini Arusha bi Esta Maganza kutowatumikisha watoto kwa kuwafanyisha biashara hasa za kuuza mifuko na kubeba mizigo sokoni.

Mtendaji huyo amesema kuwa kitendo cha jamii kujisahau na kuanza kuwafanya watoto kama watumwa wao kwa kuuza vitu mbalimbali sokoni kama mifuko ya plastiki pamoja na kuwabebesha mizigo ni kosa kisheria.

Baadhi ya watoto waliozungumza na Sunrise Radio wamesema kuwa wanafanya biashara hizo ili wapate kipato kwani wanaishi katika mazingira magumu ingawa wanajua kuwa ni kosa wao kutumikishwa.

Nao wafanyabiashara katika soko hilo la kilombero wamesema kuwa ingawa watoto hao wanatafuta riziki zao kwa nguvu zao, bado si jambo jema kuwatumikisha watoto kwani wanakosa haki zao za msingi hasa elimu.