Update:

MKUU WA MKOA DODOMA AVUNJA BARAZA LA BIASHARA NA KUTOA SIKU SABA KWA WAKUU WA WILAYA KUUNDA BARAZA JIPYAMkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodarn Rugimbana amevunja mabaraza la biashara mkoani humo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumika kisiasa.

Akizungumza jana ofisini kwake, Rugimbana amesema mabaraza yaliyovunjwa ni ya wilaya na la mkoa. Amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia uundwaji wa mabaraza hayo ndani ya siku saba.

Amesema mabaraza yatakayoundwa yalenge kutatua changamoto zilizokuwa zikiyakabili. Pia amesema mabaraza hayo anataka yasimamie uanzishwaji wa viwanda.