Update:

Matokeo ya ufunguzi msimu mpya EPL

Manchester United imeanza vema kampeni za Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2017-18, shukrani kwa Lukaku, Matic, Pogba na MartialRomelu Lukaku alitikisa nyavu za timu ya West Ham kwa mabao mawili na wakati huo wachezaji wengine wawili ambao ni Paul Pogba na Antony Martial waakihitimisha kuiadhibu timu hiyo kwa kufunga goli moja kila mmoja na kupata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya West Ham.

Timu ya Chelsea hata hivyo ilianza msimu vibaya baada ya kushindwa kuhimili makali ya klabu ya Burnley iliyoiyuka mabao 3-2 walipocheza nyumbani Stamford Bridge huku Liverpool ikitoka Sare 3-3 na timu ya Watford.

Arsenal pia ilianza vyema msimu huu baada ya kushinda Leicester City 4-3, Manchester City ikalaza Brighton & Hove Albion 2-0 ilihali Totenham Hotspurs ilirindima Newcastle United bao 2-0