Update:

Manchester United yamuongezea mkataba wa mwaka mmoja Zlatan Ibrahimovic


Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic. Ibrahimovic alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti alilolipata tangu Aprili 28.

Mchezaji huyo wa Old Trafford aliifungia timu hiyo jumla ya mabao 28 katika michezo 46 aliyocheza msimu uliopita. Mara baada ya kusajiliwa Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 alisema amerudi United kumalizia kile alichokianza. Mchezaji huyo sasa atakuwa akivaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyejiunga na Everton.

No comments