Update:

LIVERPOOL YAIGOMEA BARCELONA OMBI LA KUNYAKUA COUTINHO
Liverpool imekataa ombi la Barcelona kumasajili mchezaji wake Phillipe Coutinho kwa jumla ya Yuro milioni 100 million.Ombi la pili la Barca kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, iliyokataliwa kwa haraka ilidhaniwa kuwa ya Yuro milioni 85 itakayafuatwa na Yuro milioni 15 kama nyongeza.

Liverpool inasisitiza kuwa Coutinho – aliyejiunga na timu hiyo kutoka inter milan mwaka wa 2013 hawezi kuuzwa kwa vyovyote vile.

Barcelona ilimuuza nyota wa Brazil Neymar kuingia Paris St-Germain kwa usajili wa rekodi wa pauni milioni 200 wiki iliyopita

Coutinho alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na Liverpool januari mwaka huu.