Update:

La Liga kuingilia kati usajili wa Neymar kujiunga na PSG

Shirikisho la soka nchini Hispania limeingilia kati usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazili, Neymar Dos Santos kujiunga na Paris Saint-Germain kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 198 kiasi ambacho kinamfanya kuweka rekodi ya dunia akitokea Barcelona. Zikiwa zimesalia saa chache kuhitimisha kwa usajili huo wa Neymar kuliibuka wingu zito katika usajili huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya dunia, chama cha soka cha nchi hiyo kimesema PSG walishajaribu kutuma dau hilo kwa Barcelona ili kujaribu kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo lakini La Liga walikikataa kiasi hicho cha pesa.

Uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar umepingwa vikali na La Liga huku ikigomea sheria inayotumika kumsajili mchezaji huyo

Wanasheria wa PSG wamewasili katika shirikisho hilo (La Liga) mjini Madrid jana Alhamisi katika kuhakikisha wanazima jaribio la La Liga kumzuia mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 25.

Tayari La Liga jana ilitoa taarifa kuwa wamewasiliana na wanasheria wa mchezaji huyo.

No comments