Update:

Klabu za EPL kuamua tarehe ya mwisho ya uamisho wa wachezaji


Klabu za kandanda nchini England zinajadiliana kuhusu pendekezo la kufungwa kwa soko la kuhama kwa wachezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Kwa muda sasa, kipindi cha cha kuhama kwa wachezaji kimekuwa kikiendelea takriban wike tatu baada baada ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya Premia. Msimu huu utakuwa vivyo hivyo kwani kipindi cha uamisho itakamilika tarehe Agosti 31.


Kutokana na haya kura inatarajiwa kupigwa wakati wa mkutano wa washika dau tarehe 7 Septemba.

Tayari, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp na mwenzake wa Swansea Paul Clement wametanganza umuhimu wa kuwepo kwa mabadiliko.

Sheria za Fifa zinasema kuwa muda wa kuhamwa wachezaji unastahili kufungwa Septemba mosi.

Suala hilo limekuwa tatizo kwa baadhi ya wachezaji wa kutegemewa ambao wanatarajiwa kuhama klabu hata baada ya kushiriki mechi ndani msimu mpya.

No comments