Update:

Kesi ya upande wa upinzani kupinga matokeo ya kura za urais nchini Kenya yasikilizwaKesi ya kupinga matokeo ya kura za urais yaliyompa rais Uhuru Kenyatta ushindi imeanza kusikilizwa leo baada ya maamuzi ya awali kuhusu ushahidi uliowasilishwa na Raila Odinga, mgombea wa urais anayepinga matokeo hayo.

Jopo la wajumbe saba katika Mahakaka Kuu linatarajiwa kutoa hukumu juu ya ombi la Raila la kufungua komyuta za Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kwa ajili ya kukaguliwa, kabla ya kusikiliza mawakili wake na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka.

Odinga anaitaka Mahakama Kuu kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 8 mwezi huu, kwa madai kuwa IEBC ilishindwa kufuata sheria na kanuni katika utendaji wake.

No comments