Update:

Ibrahimovic kupewa majukumu ya ukocha ManchesterMshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 anatarajiwa kukabidhiwa majukumu mapya akikamilisha kusaini mkataba wake na Manchester United.

Taarifa kutoka klabu hiyo zinasema kwamba Kocha Jose Mourinho amepanga kumpa majukumu ya kufundisha kikosi hicho ili kuendelea kuwa na timu tishio msimu huu.

Raia huyo wa Sweeden amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili baada ya kupata majeraha wakati wa michuano ya Ligi ya Europa msimu uliopita.