Update:

HOFU YAZIDI KUTANDA KWA WAKAZI WA ARUSHA KUFUATIA UONGEZEKO LA MATUKIO YA UTEKAJIUtata umeendelea kuwagubika wananchi mkoani Arusha kufuatia kuongezeka kwa utekwaji wa watoto ambapo mpaka hivi sasa watoto sita hawajulikani walipo .

Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi wamesema kuwa kumekuwa na fununu kuwa watekaji hao wamekuwa wakiacha ujumbe kuwa waletewe kiasi cha fedha ili watoto wao warudishwe wakiwa hai.

Hofu hiyo imebainishwa na wenyeviti wa mitaa kutoka maeneo tofauti tofauti mkoani hapa ambako katika maeneo yao ndiko matukio hayo yamekithili na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuondoa hofu hiyo.

Kwa upande wa jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia kwa kamanda Charles Mkumbo amekiri kuyafahamu matukio hayo na kutoa rai kwa wazazi kuwa endapo watoto wao watapotea wawahi kituo cha polisi kutoa taarifa.

No comments