Update:

David Eldar bingwa mpya wa mchezo wa Scrabble


Bingwa mpya wa mchezo wa kuunda maneno kwa kutumia herufi maarufu kama Scrabble ametawazwa. David Eldar, 27, alishinda taji hilo baada ya kuandika neno "carrels" - aina ya chumba kidogo chenye meza, sana ambavyo hupatikana kwenye maktaba katika vyuo vikuu kumuwezesha mtu kusoma vitabu akiwa faraghani.Neno hilo lilimzolea Eldar alama 74 na kumshinda mpinzani wake Harshan Lamabadusurilya 3-0 katika fainali iliyokuwa na michuano mitano.