Update:

Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kuwekeza kiasi cha Dola milioni 4.2 Kituo cha Usambazaji umeme cha Njiro


Mradi wa umeme katika Kituo cha kupoozea umeme cha Njiro kilichoko Mkoani Arusha chenye uwezo wa kuzalisha megawati 130 unatajwa kuwa msaada kwa wakazi wa Arusha kwani utapunguza kwa kiasi kikubwa adha ya umeme kukatika.

Hali hiyo inatokana na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kuwekeza kiasi cha Dola milioni 4.2, ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili kuongeza uwezo wa Kituo hicho kuzalisha umeme unaotumika kwa ajili ya makazi ya watu, maeneo ya biashara na viwanda.

Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Usambazaji umeme cha Njiro Mhandisi Lembrice Mollel amesema mradi huo   umesaidia kuongeza Megawati 130 za umeme hivyo kukidhi mahitaji ya Jiji la Arusha kiasi cha Megawati 60  na kuwa na ziada ya megawati 70.


Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Umeme wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Frorence Gwang’ombe amesema kuwa lengo la mradi lilikuwa kupatikana kwa umeme wa uhakika .

No comments