Update:

Arsenal yatamba baada ya kutwaa Ngao ya Jamii


Klabu ya Arsenal jana ilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuishinda Chelsea kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamnii uliopigwa katika uwanja wa Wembley.

Arsenal ilipata ushindi huo baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea ambao walikuwa wa kwanza kupata bao la kuondoza dakika 46 likifungwa na Victor Moses lakini Arsenal walisawazisha kupitia kwa mchezaji aliyesajiliwa karibuni kutoka klabu ya Shalke ya Ujerumani Sead Kolasinac dakika ya 82.

Arsenal ilifunga mikwaji yake yote ya penalty huku Chelsea ikishinda penalty moja tu kupitia nahodha Gary Cahill. Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois alishindwa kufunga penalti yake, akifuatwa na mshambuliaji aliyenunuliwa karibuni kutoka Real Madrid ya Uispania Alvaro Morata waliopiga nje.

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud alifunga penalti ya mwisho na kuhakikisha arsenal imeshinda taji la Ngao ya jamii kwa mara nyingine. Wengine waliofungia arsenal ni Theo Walcott, Nacho Monreal na Alex Oxlade Chamberlain.