Update:

7 wakamatwa kwa wizi wa umeme ArushaWatu 7 wamekamatwa mkoani hapa kwa tuhuma ya kujiunganishia umeme kinyemela. Kwa mujibu wa Shirika la umeme mkoa wa Arusha limesema kuwa kukamatwa kwa watu hao kunatokana na msako unaoendelea wa kuwakamata wezi wa umeme .

TANESCO wamesema kuwa wezi hao si tu wanaohujumu shirika bali wanaweza kusababisha madhara makubwa kwani wanapojiunganishia umeme hutumia mbinu zinazoweza kusababisha moto ama kuugua kwa vitu.

Msako huo umefanyika usiku katika maeneo mbalimbali ya mji mdogo wa Ngaramtoni na Ilkiding'a , zoezi ambalo afisa usalama wa TANESCO mkoani hapa wanasema ni endelevu .

Akizungumzia athari za miundombinu ya shirika inayosababishwa na uunganishaji huo holela ,mdhibiti wa mapato wa shirika hilo mhandisi Hassan Lumuli amesema mashine za Transfoma ndizo zinazoathirika zaidi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji tofauti na idadi iliyopangwa.