Update:

Wizara ya Mambo ya Ndani yakanusha uzushi kuhusu sheria


Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma kuwa kumekuwepo na taarifa za uongo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha Habari kinachosema “Kanuni/Sheria za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Taarifa hizo zimeanza kusambazwa kuanzia jana tarehe 18 Julai 2017 zikidai kuwa kuanzia tarehe 19 mwezi Julai Mwaka 2017 na kuendelea kutakuwa kuna Kanuni mpya za Mawasiliano.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na uzushi na haina ukweli wowote na inalenga kuwavuruga wananchi hivyo wananchi waipuuze taarifa hiyo.

Wizara inatoa onyo kali kwa mtu yeyote aliyeanzisha na wale wanaoendelea kusambaza taarifa hiyo na pia hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaozusha mambo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Serikali inao mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa kwa kutumia mfumo wa “kielectroniki na hardcopy’’.

Imetolewa na

Christina R. Mwangosi

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.