Update:

WAUMINI WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA UBATIZO WA MAJI MENGI WILAYANI ROMBO
Waumini wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio hilo lililotokea JANA Julai 16 saa sita mchana.

Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini anayedaiwa alipandisha mapepo; alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.

Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na kuwasababishia kifo. Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa kwa kufanya Ubatizo huo kwenye kina kirefu cha mto huo.

No comments