Update:

WANANCHI WILAYANI BABATI WALIA NA ADHA YA KUTOKUKAMILIKA KWA LAMBO LA KUNYWESHEA NG'OMBE

Wananchi wa kijiji cha Sangaiwe Kata ya Mwada  wameiomba Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara kukamilisha ujenzi wa lambo la kunyweshea mifugo .

Wakiongea na waandishi wa Habari wananchi hao walidai kuwa lambo hilo lilijengwa mwaka wafedha 2008/2009 kwa gharama ya shilingi milioni 70  na kwamba toka lijengwe lilitumika kwa miaka miwili tu kisha miaka iliyofuatia lilishindwa kuhifadhi maji kwakuwa lilikuwa limejaa tope.

Wamesema kuwa ingawa wao si wataalamu waliochimba lambo hilo  lakini kama watu wenye akili timamu wanaona kuwa wachimbaji hawakufanya kazi ipasavyo kwani ni kama walisogeza udongo pembeni tu badala ya kuchimba.

Kwa upnde wake Diwani wa Kata ya Mwada Gerald Chembe alieleza kuwa suala la utatuzi wa  tatizo la maji utakamilika pale  tu chanzo cha maji  cha Mto DARAKUTA kitakapoboreshwa.


Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Onesmo Mwakasege alifafanua kuwa katika mwaka wa fedha  wa 2008/2009  fedha iliyotengwa kwa ujenzi wa lambo hilo ni shilingi milioni 320 ambapo Halmashauri ya Wilaya ilipokea milioni 60kwa ajili ya ujenzi wa lambo hilo.

No comments