Update:

Wanajeshi wa kulinda amani waongeza kambi zao DRC


Naibu wa Kamanda wa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza habari ya kufunguliwa kambi nyingine nne za kijeshi za askari hao katika mikoa miwili ya katikati mwa nchi hiyo.

Afisa huyo wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa amesema hayo mjini Kinshasa na kuongeza kuwa, uamuzi wa askari hao kuongeza idadi ya kambi zao za kijeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umechukuliwa baada ya kushadidi mapigano baina ya makundi hasimu katika mikoa ya Kasai na Kasai Katikati.Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoAmesema, zoezi la kuanzisha kambi hizo nne katika mikoa hiyo miwili limeanza kutekelezwa na kwamba kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kina mpango wa kuanzisha makundi madogo madogo ya wanajeshi na kuyatuma kwenye maeneo mengi ya nchi hiyo ili kulinda amani.

Tangu mwaka jana hadi hivi sasa, mkoa wa Kasai wa katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na maeneo mengine matatu ya karibu na mkoa huo yamo katika machafuko na mapigano baina ya makundi hasimu.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Algeria na ina watu milioni 72 na utajiri mkubwa sana wa maliasili.

No comments