Update:

WAFANYABIASHARA WALIO MWAGIWA TINDIKALI WAAMISHIWA KCMC KWA MATIBABU ZAIDI
Wafanyabiashara wanne wa madini waliomwagiwa kemikali machoni wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyoko mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya.

Wafanyabiashara hao ni pamoja na Sabas Laiser, Lucas Soto, George Nyakiha, Moringe Mollel pamoja na mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo mkoani hapa, Ngalama Mapera.

Akizungumza na waandishi wa habari JANA mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Dk Jackline Urio amesema kwamba waliwapokea majeruhi hao juzi na kisha kuwapatia huduma ya kwanza kwa kuwaosha macho.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwamba jeshi hilo mkoani hapa limefanikiwa kuwashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo

No comments