Update:

Usajili ligi kuu Uingereza: Mourinho asema hafurahishwi na usajili unavyoendeleaMeneja wa Manchester United Jose Mourinho amedaiwa kutofurahishwa na taratibu za usajili unavyoendelea wa msimu huu katika klabu yake. Baada ya Manchester kutwaa taji la michuano ya ligi ya Europa, meneja huyo alisema alimpa makamu mwenyekiti wa timu hiyo orodha na wachezaji anaowahitaji kusajili.

Mourinho anahitaji mshambuliaji mmoja atakayeziba pengo la Zlatan Ibrahimovic pamoja na kiungo mkabaji. Man U imekuwa ikimuwania mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambaye hatma ya uhamisho wake bado haujulikani.

No comments