Update:

UN yawatuhumu wanajeshi wa DRC kuhusika na mauaji ya KasaiUmoja wa Mataifa umelituhumu kwa njia isiyo ya moja kwa moja jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa limehusika na mauaji ya umati katika eneo la Kasai.

Ripoti ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kongo (UNJHRO) imesema aghalabu ya makaburi ya halaiki yaliyogunduliwa katika eneo la Kasai yalichimbwa na 'maafisa fulani' wa jeshi la Kongo DR.

Hii ni mara ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kulihusisha moja kwa moja jeshi la DRC na mauaji ya umati katika eneo la Kasai, katikati mwa nchi hiyo ya Kiafrika.Moja ya makaburi ya umati eneo la Kasai, DRC

Mapema mwezi huu, ofisi hiyo ya UN ilitangaza kugundua makaburi mengine 38 ya umati magharibi mwa Kasai, na kufikisha idadi ya makaburi hayo yanayodaiwa kuchimbwa na jeshi la Kongo DR katika eneo hilo kufikia 80.

Watu zaidi ya 3,300 wameuawa huku wengine milioni 1.4 wakifurushwa katika makazi yao tangu mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, katika mapigano baina ya wanamgambo wanaomuunga mkono Kamwina Nsapu, kiongozi wa kundi la waasi katika eneo hilo na askari wa serikali ya nchi hiyo.

No comments