Update:

Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa wafanyika Jamhuri ya Congo


Uchaguzi wa bunge na wa serikali za mitaa umefanyika jana nchini Jamhuri ya Congo.
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo imesema vituo zaidi ya 5000 vya kupiga kura vilifunguliwa jana kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni, lakini ulichelewa kuanza katika mkoa wa Pool kutokana na sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tume hiyo, wagombea 711 watagombea viti 151 kwenye bunge la nchi hiyo, na wagombea 8,131 watagombea viti 1158 vya wawakilishi wa serikali za mitaa.

No comments