Update:

Taifa Stars kushiriki mechi ya marudio na Rwanda kuamua mshindi

Taifa Stars kushiriki mechi ya marudio na Rwanda kuamua mshindiMkufunzi wa timu ya soka ya Rwanda Amavubi Stars Antoine Hey amewapongeza wachezaji wake baada ya kutoka sare kwenye mechi baina yao na Tafa Stars ya Tanzania kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mechi hiyo ilikuwa raundi ya kwanza ya mchuano wa kufuzu mashindano ya CHAN mwakani na kocha huyo mjerumani anataka kikosi chake kuboresha matokeo na kujikatia tikiti katika mechi ya marudiano itakayoandaliwa Kigali Rwanda siku ya jumamosi kwa kushinda Tanzania.
Mshindi wa mchuano huo atakutana na Sudan Kusini au Uganda katika raundi ya tatu, baada ya timu hizo kutoka sare tasa katika mechi yao ya kufuzu siku ya Jumamosi mjini Juba.