Update:

Polisi wa Kenya wavunja jaribio la shambulizi la Al-Shabaab mjini Lamu


Vikosi vya usalama vya Kenya jana vilivunja jaribio la shambulizi la Al-Shabaab mjini Lamu, saa kadhaa baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la kuimarisha mapambano dhidi ya magaidi kwenye sehemu hiyo.

Ofisa wa polisi amethibitisha habari kuhusu kuvunjwa kwa jaribo la shambulizi hilo, na kusema magaidi karibu 30 wenye silaha walikuwa wanajaribu kushambulia kambi ya polisi ya Mokowe na kukimbia baada ya kuona kuna askari wa usalama.

Mashuhuda wanasema magaidi hao walirudi katika msitu mkubwa wa Boni, wanaotumia kama maficho yao na kufanya mashambulizi dhidi ya vijiji vya Lamu.