Update:

Mmiliki wa Impala afariki dunia



Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye
matibabu nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo
akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.
Akihojiwa na gazeti hili Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu
jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.
Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado
hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.
Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo
Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

No comments