Update:

Malinzi asema uongozi mpya utarejesha imani TFF
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF aliyeondolewa madarakani Jamal Malinzi amewapongeza serikali, wadhamini na wadau wote wa soka nchini Tanzania kwa msaada wao ambao anasema umesaidia kuinua viwango vya michezo nchini humo.

Malinzi, ambaye anazuiliwa kwa sasa kwa shtaka la kujihusisha na ulaghai, amejiondoa katika uchaguzi wa TFF utakaofanyika karibuni, baada ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa PCCB kumshika, likidai mashtaka kadhaa dhidi yake yakiwemo ufujaji wa pesa na matumizi mabaya ya mamlaka.

Rais huyo wa zamani wa TFF sasa amewatakia kila la heri wote watakaoshiriki uchaguzi huo wa Agosti 12 jijini Dodoma. Malinzi amesema uchaguzi huo ni wa maana sana kwani utapisha rais mpya ambaye atafungua ukurasa mpya katika uongozi wa kandanda Tanzania.

No comments