Update:

Levy alalamikia viwango vya fedha vinavyotumika kwa usajiliMwenyekiti wa klabu ya Totenham Hotspurs ya Uingereza ametetea uamuzi wa klabu hiyo ya kutoingia kwenye soko la uamisho sawia na vilabu vingine nchini humo akidai kuwa viwango vya pesa vinavyotumika kusajili wachezaji wapya si vya kuridhisha.

Zaidi ya millioni 850 pauni ya Uingereza imetumika kuwasajili wachezaji wapya baina ya timu zinazoshiriki ligi ya primea katika kipindi hiki cha uamisho itakayokamilika Agosti 31. Hata hivyo Totenham haijasajili mchezaji yeyote kinyume na matarajio ya wengi.

Levy anasema lazima fedha za vilabu vitumike vyema huku akilalama kuwa shughuli inayoendelea ya usajili kwa sasa huenda ikaleta mgogoro wa kifedha baadaye. Amehoji kuwa itakuwa vigumu kwa baadhi ya vilabu kuwalipa wachezaji idadi ya mishahara wanaowalipa wakati wa kusaini mikataba nao. Kulingana na kampuni maarufu ya uhasibu ya Deloitte, vilabu vya premia viko njiani kupitiliza rekodi ya billioni 1.165 pauni za Uingereza zilizotumika msimu iuliopita wa uamisho.

No comments