Update:

Kocha wa Taifa Stars asikitikia kubanduliwa kwa timu yake


Mkufunzi wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chake kilikuwa na bahati mbaya baada ya kubanduliwa nje ya kombe la mabingwa Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN na timu ya soka ya Rwanda Amavubi Stars siku ya Jumamosi. Timu hiyo ya Tanzania ilibanduliwa kutoka mashindano hayo kwenye raundi ya pili kwa kupitia kanuni ya bao la ugenini.
Mayanga na msaidizi wake Fulgence Novatus walidai kuwa mwachezaji wa Tanzania hawakuwa na bahati nzuri wakati wa mchuano huo, jambo ambalo walidai ilichangia matokeo mabaya ya timu hiyo.
Kwa maoni yao, Taifa stars ilisakata mpira kwa ustadi na kujitengenezea nafasi murwa kufunga mabao hila hilo halikufanyika.

No comments