Update:

FIFA Kombe la Mabara: Ujerumani yatwaa ubingwa wa mabara
Bao la dakika ya 20 lililofungwa na Larsi Stindi liliimaliza kabisa Chile na kuwafanya ujerumani kubeba ubingwa wa michuano ya kombe la mabara kwa mara ya kwanza.

Chile walionekana kupambana kwa nguvu zote kutaka kusawazisha lakini juhudi za mlinda mlango wa Ujerumani Adre Ter Stegen alikuwa kikwazo.


Ureno wenyewe wamejikuta wakikamata nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mexico goli 2-1.

Ujerumani imechukua kombe kutoka kwa Brazil ambao walikuwa wakilishikilia