Update:

Everton yatua Dar es Salaam tayari kukabiliana Gor Mahia ya Kenya


Wachezaji wa klabu ya Everton ya England wako jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara yao ya kwanza kabisa Afrika Mashariki. Wachezaji hao na wakufunzi pamoja na maofisa wengine wa timu walipokelewa kwa mbwembwe baada ya kuwasili kutoka Liverpool. Ziara yao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Premia, Uingereza. Miongoni mwa wachezaji waliosafiri Tanzania ni Wayne Rooney ambaye amerejea katika klabu baada kuwa Manchester United. Mashabiki wengi wa soka wamefika Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam baadaye siku ya leo.Image result for evaton yatua dar