Update:

Costa atemwa nje ya kikosi cha Chelsea

Mshambuliaji wa Uispania Diego Costa atakosa ziara ya maandalizi ya msimu ujao ya klabu ya Chelsea huku kukiwa na madai kwamba mchezaji huyo ataondoka Stamford Bridge.
Chelsea itaanza ziara ya China baadaye siku ya leo lakini mkufunzi Antonio Conte hakumjumuisha costa na mwenzake Nemanja Matic katika kikosi chake.
Costa mwenye umri wa miaka 28 ameelezea nia yake ya kurejea Atletico Madrid ingawa klabu hiyo imepigwa marufuku kushiriki katika uhamisho.
Raia wa Serbia Nemanja Matic anadaiwa kusakwa na baadhi ya vilabu kutoka Uropa zikiwa ni pamoja na mahasimu wa Chelsea, Manchester United.
Tom Wanjala anazungumza na Simon Mwangi Mchambuzi wa Michezo.

No comments