Update:

Beki wa Monaco Benjamin Mendy ajiunga na Manchester CityBenjamin Mendy amekamilisha uhamisho wake wa millioni 52 pauni ya Uingereza kutoka mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa AC Monaco na kuingia Manchester City.

Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya Uingerezana na kuwa beki wa bei ghali mno kwenye ligi kuu ya premier.

Mendy ni mchezaji wa tano kusajiliwa na City kwenye msimu huu wa uhamisho, na kufikisha matumizi ya fedha zake millioni 200 pauni ya Uingereza.

Mchezaji huyo aliichezea Monaco mechi 34 msimu uliopita na kuisaidia kunyakua kombe la Ligue 1 kwa mara ya kwanza kwa miaka 17 iliyopita baada ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Marseille.