Update:

AFARIKI KWA KULA MIHOGO YENYE SUMUMTU mmoja amefariki dunia na wengine wanne wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Masigati,wilayani Manyoni Mkoani Singida wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni,baada ya kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni,Bi Elizabeth Akunay amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja aliyefariki wakati akipelekwa kwenye matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni kuwa ni Saidi Ramadhani aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.


Kwa mujibu wa Muuguzi huyo watoto waliopokelewa katika Hospitali hiyo julai,19,mwaka huu saa mbili za usiku wakiwa na hali mbaya ni pamoja na Christopher Ramadhani,Happyness Ramadhani,Juma Ramadhani na Joyce David wote ni wakazi wa Kijiji cha Masigati.Hata hivyo Muuguzi huyo ametumia fursa hiyo kuwashauri wazazi na walezi wa watoto wajaribu kuonja vyakula kabla ya kuwapa watoto wao ili kuepusha matukio ya vifo huku wakisisitiza kutolewa kwa elimu kwa akina mama itakayowasaidia kujua vyakula vizuri au vibaya.

No comments