Update:

Yanga SC yakwamia nusu fainali michuano ya Sportpesa Super Cup

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Yanga SC wameshindwa kuonyesha ubabae mbele la AFC Leopards na kushindwa kutinga Finali kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 4- 2  kete yao ya pili wameirusha mapema leo  tarehe 8/06/2017 kwenye  michuano ya Sportpesa Super Cup dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika viwanja vya UHURU stadium jijini Dar es Salaam  huku macho ya watanzania yakiwa kwa timu hiyo yakitegemea  kama ingeweza  kuleta ubingwa nyumbani .
Timu ya Yanga ndiyo timu pekee iliyoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Simba SC, Singida United na Jang’ombe ya Zanzibar kutolewa mapema katika hatua ya robo fainali ya michuano yenye mvuto wa aina yake.
Katika mechi za  timu ya AFC Leopards  imejikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup 2017 kuwania kitita cha Dola za kimarekani 30,000.