Update:

WANANCHI WA SENGEREMA WAELEZEA JINSI TATIZO LA MAJI LINAVYOWATESA


Wananchi wa kijiji cha Isebwa na kijiji cha Tunyenye kata ya Kishinda wilayani Sengerema mkoani Mwanza wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.

Wakizungumza na MO Blog wananchi hao wamesema tatizo la maji katika maeneo yao limekuwa ni mwiba kwani hulazimika kuamuka usiku wa manane na kutembea umbali mrefu kwenda kusaka huduma hiyo.

Kutokana na kadhia hiyo wananchi hao wameamua kupaza kilio chao hicho mbele ya diwani wa kata hiyo Silvanus Bulapilo ili watatuliwe kero hiyo kwani inachangia kusimamisha shughuli zote za maendeleo kwa wakazi hao na kubaki wakiwaza suala moja pekee la maji.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo, Silivanus Bulapilo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema amekiri kuwepo na changamoto katika maeneo hayo na kusema kwa sasa tayari wameshaingia mkataba na mkandarasi wa kuchimba visima vya maji katika kijiji cha Tunyenye.

Aidha diwani huyo amesema serikali inatambua adha wanazozipata wananchi hivyo watahakikisha wanatatua kero hizo katika maeneo mbalimbali ili kuwaondolea usumbufu wanaoupata wananchi wa kuamka usiku wa manane kutafuata huduma hiyo muhimu ya maji

No comments