Update:

WAKULIMA WA BANGI WAKIRI KUACHA KULIMA ZAO HILO NA KUFYEKA ZAIDI HEKARI 400 KIJIJI CHA KISIMIRI JUU WILAYA YA MERU


By Michael Nanyaro


Baada ya kufanya kilimo haramu cha zao la bangi kwa kipindi kirefu wananchi katika kijiji cha kisimiri juu wilayani Arumeru mkoani Arusha wameridhia kwa pamoja na kuamua kuachana na kilimo hicho kwa kuyafyeka mazao hayo ya bangi kwa zaidi ya ekari mia nne na kuahidi kuachana na kilimo hicho kwani wamechoka kuishi kwa mashaka.Wakizungumza na Mwandishi wa wetu  baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakiwa katika zoezi la kuendelea kuyafyeka mazao hayo ambapo wameeleza kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakikosa huduma za kijamii kutokana na kuendelea kufanya kilimo hicho pamoja na kuish kwa mashaka hali ambayo inasababisha hathari kwa familia zao na kuamua kuachana na kilimo hicho.

Pamoja na wananchi wa kijiji hicho kueleza uamuzi wao huo wa kupanda bangi na kuamua kuzifyeka kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na kukiri uchumi wa wananchi wake kushuka kutokana na kuachana na kilimo hicho akazungumzia nia yao ya kuachana na kilimo hicho cha bangi.Aidha afsa kilimo wa halmashauri ya Meru Liberatus Msasa akatoa ushauri kwa wananchi hao kuanza kufanya kilimo cha Pareto,mbaazi pamoja na viazi.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru akisimamia zoezi la uchomaji wa bangi zaidi ya hekari 400

Wille Joseph Njau ni mwenyekiti wa halmashauri ya Meru ambaye aliweza kufika katika kijiji hicho na kuwapongeza wananchi hao kwa maamuzi ya kuachana na kilimo hicho.


Wananchi katika kijiji cha kisimiri juu katika Kata ya Uwiro wamekuwa wakijihusisha na kilimo hicho kwa muda mrefu ambapo kijiji hicho kina zaidi ya wananchi 5000 ambapo baadhi wamekuwa wakilima bangi na kuziuza huku wakiishi katika mazingira magumu

No comments