Update:

Vita ya Real Madrid na Manchester United katika usajili yachukua sura mpya
Vita kati ya Real Madrid na Manchester United katika usajili imechukua sura mpya baada ya Real Madrid nao kulipiza kile ambacho Manchester United waliwafanyia kwa mlinda mlango wao David De Gea.

Wiki iliyopita kuliibuka taarifa kwamba Real Madrid walijaribu kutuma ofa kwa Manchester United kwa ajili ya De Gea lakini United waliikataa ofa hiyo na kuwaambia Real Madrid waongeze dau hadi euro milioni 66.

Wiki hii nayo United wametuma ofa kwa Real Madrid kujaribu kumsajili mshambuliaji wao Alvaro Morata ambaye tayari amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kocha Zinedine Zidane.

Manchester United wametuma ofa ya euro ml 52 lakini Real Madrid wamekataa kiasi hicho cha pesa na kuwaambia wakaongeze tena euro 26.6m ili kumpata Alvaro Morata ambaye pia anafukuziwa na Chelsea na Ac Millan.

Jose Mourinho anapambana sana kutafuta mshambuliaji mkubwa lakini madau yao yamekuwa hayashikiki, Mourinho anamtaka Lukaku ambaye habari zinadai anarudi Stamford Bridge lakini pia Mourinho anafuatilia kwa makini sahihi ya Andrea Belotti wa Torino. Bado haijfahamika kama Mourinho atatuma ofa nyingine kwa Real Madrid au ataachana na mpango wa kumnunua Morata ama huenda akamtumia David De Gea kama sehemu ya kumnasa Alavaro Morata.

No comments