Update:

Usain Bolt aaga mashabiki nchini JamaicaUsain Bolt ameaga mashabiki wake wa nyumbani huko Kingston kwa kushinda mbio za mita 100. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ataaga rasmi mchezo huo mwezi Agosti mwaka huu baada ya mashindano ya World Championship mjini London.

Bolt alikimbia kwa kasi ya sekunde 10:03 mbele ya mashabiki 30,000 waliocheza dansi huku wakipeperusha bendera na kurusha fataki ikiwa ni ishara ya kumuaga.

No comments