Update:

UEFA yabuni Tuzo 5 mpya za wachezaji bora wa mwaka
UEFA imetangaza kuanza kutolewa kwa tuzo 5 mpya za wachezaji bora wa mwaka kuanzia Agosti mwaka huu ambazo washindi wake watapatikana toka kura za makocha na wanahabari.

Tuzo hizo zitakabidhiwa huko Monaco hapo Agosti 24 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA Champions ligi

Tuzo hizo 5 mpya ni kwa wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano ya klabu ya UEFA kwa msimu uliopita, yaani ule wa 2016/17, na zitatoka sambamba na zile za sasa za mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake.

No comments