Update:

Tyson Fury amtambia Anthony Joshua na kutaka kuzichapa naye

Bondia wa Uingereza katika uzani mzito duniani Tyson Fury anataka kuzichapa na Anthony Joshua ambaye ana asili ya Nigeria.

Katika kanda ya video iliyochapishwa katika mtandao wa You Tube, Fury anasema kwamba yeye ndio ‘njozi mbaya’ ya Anthony Joshua.

Tayari alishakubali kupigana na Joshua baada ya ushindi wake dhidi ya Wladmir Klitschko.

Joshua ambaye alimpiga knockout raia huyo wa Ukrain katika raundi ya 11 katika uwanja wa Wembley baada ya pigano hilo alimtaka Tyson Fury ambaye pia alimshinda Klitschko katika pigano jingine.

No comments