Update:

Turan wa Bacra afukuzwa timu ya Taifa kwa kumtwanga muandishi Kiungo wa Barcelona


Arda Turan amestaafu soka ya kimataifa baada ya kuenguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uturuki kwa kosa la kumpiga muandishi wa habari kwenye ndege akiwa na timu yake ya taifa wakirejea kutoka Skopje ambapo Uturuki ilitoka sare ya 0-0 na Macedonia.

Mchezaji huyo mwenye miaka 30, kiungo wa Barcelona, ambaye amechezea Uturuki mechi 96, amesema anaona sasa ni wakati wake wa kuhitimisha safari yake ya kuchezea timu yake ya Taifa.