Update:

TOZO KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO KUANGALIWA UPYA

Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.

Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.

No comments