Update:

TANAPA KUCHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA MADARASA BAKWATA

Image result for TANAPA

SHIRIKA la hifadhi za Taifa (TANAPA)limeahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa baraza la waislamu BAKWATA wilaya ya Arumeru kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la madrasa katika msikiti wa mji mwema.

Akizungumza na viongozi wa baraza hilo ofisini kwake katika hafla fupi ya kukabidhiwa cheti cha pongezi kwa mchango wa Tanapa kusaidia ujenzi wa jengo hilo, mkurugenzi wa shirikika hilo,Allan Kijazi alisema kwamba shirika lao limekuwa na utaratibu wa kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo elimu kwa lengo la kuunga mkono sera ya serikali .


Awali akizungumza kwa naiba ya viongozi wa Bakwata wilayani Arumeru mwenyekiti wa baraza hilo wilayani humo, Sheikh Haruna Husein ameshukuru kwa msaada huo na kusema kuwa Madrasa hiyo itasaidia kuwakuza kielimu na kimaadili watoto ambao ndio viongozi na raia wema wa baadae.

No comments