Update:

Sportspesa Super Cup: Yanga na AFC Leopard zatinga nusu fainali


Timu ya Yanga ya Tanzania na AFC Leopard ya Kenya zimefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup michezo iliyopigwa jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es salaam.
Yanga imeing'oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.
Image result for SPORT PESA SUPER CUP
Nayo AFC Leopard imeifgunga Singida United kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1.
Sasa Yanga itakutana na AFC Leopard. Michuano hiyo inaendelea leo kwa kuzikutanisha timu ya Simba Sports Club ya Tanzania itakutana na Nakuru All Stars ya Kenya, huku Gor Mahia itakapomenyana na Jang'ombe Boys ya Zanzibar.

No comments