Update:

Sababu 5 ambazo zinaweza sababisha kukosa ajira (baada ya interview)


Je umenda kwenye mahojiano ya kazi mengi, bila kufanikiwa kupata ajira? Je unataka kujua sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kutokupata ajira baada ya interview? Katika nakala hii tutakupa sababu 5 zinazo sababisha mtu kutokupata kazi mdaa mwingi baada ya interview.
Mavazi Mabaya:

 Jinsi utakavyo vaa ukienda kufanya mahojiano ya kikazi ni kitu mwajiri anakizingatia sana. Kama ukienda kwenye interview umevaa labda kaptura au labda nguo imechanika, mwajiri anaweza hata asikusikilize na akakuambia uondoke tu. Na hata kama akikubali kukufanyia interview ukitoka hapo huto pigiwa simu ya kurudi. Inabidi uhakikishe unavaa nguo ambazo zinafaa kuvaa ofisini.
Kutokuwa umejiandaa kwajili ya interview:

 Usiende kwenye interview bila kujua vitu kuhusu nafasi ya ajira uliyoiomba na pia kuhusu kampuni inayo ajiri. Makampuni mengi lazima waulize maswali yanayoendana na hayo mambo mawili. Ukishindwa kujibu maswali kuhusu hivyo vitu, hutopata hiyo kazi. Pia kuna swali lazima ulizwe kwenye kila interview: Tueleze wewe ni nani? Inabidi uweze kujielezea bila kubabaika. Ina muonyesha mwajiri kama unajiamini.
Kutokuwa na Sifa za kazi:

 Mara nyingi mtu unatuma maombi ya kazi kila sehemu bila kusoma maelezo kuona kama una faa kufanya kazi hiyo. Inabidi uwe unatuma maombi sehemu amabazo unaona kwamba kazi unaweza kuifanya na pia una sifa za hiyo kazi. Kama kazi ni ya uhasibu na wewe hujasomea uhasibu, ukituma maombi mwajiri hato kuita kwenye interview.
Unakosa Ujasiri:

 Unaweza ukawa na CV nzuri, ukawa unaongea vizuri kwenye simu na ukaenda kwenye interview na mavazi mazuri, ila ukashindwa kuajiriwa kwasababu yaku feli interview ya uso kwa uso. Lazima uwe mjasiri ukienda kwenye interview, hakikisha una muangalia machoni mtu anayekufanyia interview. Usiwe una aibu.
Kushindwa kujieleza:

 Wakati unaenda kwenye interview, inabidi ujieleze vizuri ila pia hakikisha unaweza kufafanua jinsi utaisaidia kampuni kukua. Ukiwa unaongea sana kuhusu wewe na husemi utaisaidiaje kampuni, mwajiri anaweza akaona hufai.